How to get free YouTube subscribers, likes and views?
Get Free YouTube Subscribers, Views and Likes

Jux : 'Nilikaa Na Jackie Mwezi Mzima China Akawa Hapatikani Sikumuona Tena' | SALAMA NA JUX PT 2

Follow
YahStoneTown

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

Juma Jux ni mtanashati haswa hicho ndicho cha kwanza na suala la yeye pia kuwa muimbaji mzuri (na anayeendelea kujengeka) kunamfanya pia awe wa kipekee, anajua maana halisi ya kufanya kazi kwa bidii ili uweze kutimiza malengo ambayo wewe unakua umejiwekea. Ana aibu pia sana ila hili unaweza ukalitilia shaka kwasababu ya kazi aliyoamua kuichagua. Kwa nilivyo muelewa mimi yeye aliamua kufanya muziki kwasababu rafiki zake walikua wanafanya muziki na zaidi akiamini yeye ni Rapper kuliko hata kuwa muimbaji.

Kwa mujibu wake kwenye kundi lao hilo la shule yeye ndo alikua sio mkali na wala hakua na neno juu ya hilo, zaidi yeye alikua anataka ku fit in zaidi. Lakini leo hii yeye ndo mwenye mafaniko zaidi kwenye fani yake kuliko wale walokua ndo wakali wa kazi hizo wakati bado wako shuleni. Jux ananiambia mpaka leo wanaendelea kuwa marafiki na rafiki zake wa shule, zaidi Cyrill Kamikaze ambaye amekua kama ndugu yake. Pia anakumbuka mara ya kwanza wimbo wake ulipoenda redioni bila ya matarajio yake na wakati anaambia B12 ameupenda na angependa akutane nae anasema baridi na uwoga na aibu aliyokua anasikia ni Mungu pekee ndo anajua.

Uzuri pia Jux ana muonekano mzuri na utanashati wake umekua ukimfanya ajikusanyie mashabiki wengi haswa wanawake na ku inspire vijana wengi watake kupita kwenye nyendo zake ili nao waweze kuja kuwa kama yeye siku moja. Combination yake na Bob Maneke nayo ni kitu ambacho kimemfanya Jux aendelee kuwa pale. Wanafahamiana vizuri na kazi ambayo wamekua wakiifanya pamoja imekua ikijieleza yenyewe.

Jux anakumbuka utanashati na kujituma kwa Marehemu Baba yake ambaye kwa maelezo yake anasema alikua Baba BORA sana, kwanza hakuwahi hata siku moja kumuona Mzee wake na Mama yake wanagombana na siku zote alikua anahakikisha watoto wake wanaishi na kusoma vizuri, nadhani nia yake ilikua kutaka kuwaona watoto wake wakiwa wasomi labda na kufanya kazi za maana zaidi au kuishi maisha mazuri zaidi kuliko yeye wakati anakua. Jux ana kumbuka Mzee wake kama mtu wa kujituma sana ambaye alijichanga kumfikisha mkewe mjini baada ya kupata kazi, yeye alikua tu fundi wa magari ila baada ya mke wake kupata kazi mjini, alihakikisha anafika na mambo mengine yaende kwa uzuri kama ambavyo alikua akiyataka kwa wanawe.

Mama yake pia humuambia zaidi siku hizi za karibuni baada ya Jux kuanza kung’ara kwenye muziki na biashara zake, Mama yake anamuambia anamkumbusha mno Marehemu mume wake na anajua fika kama angekua hai basi angekua anajivunia yeye kupita kiasi. Uvaaji wake na utanashati na jinsi ambavyo anajituma hivyo vyote Juma Jux amerithi kutoka kwa Marehemu Mzee wake. Mwenyezi Mungu Aendelee Kumpumzisha kwa Amani.

Mapenzi yake ya dhati ambayo huyaonyesha kwa watu ambao amekua nao katika mahusiano nae pia kwa kiasi kikubwa amechukua kutoka kwa wazazi wake, jinsi ambavyo Baba yake alivyokua anampenda Mama yake, ni kitu ambacho Juma amekua akikikubali sana. Na yoyote ambaye anakua nae amekua akifanya analoweza ili waendelee kudumu. Mwenzetu amekua na mwalimu mzuri sana.

Kwa akili ya muziki na biashara nadhani tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa kijana huyu hodari wa ki Tanzania. Hivi karibuni brand yake ya African Boy imetia makubaliano na kampuni moja kutoka China ambayo wamekua wakimuona Juma anafanya biashara hiyo tokea akiwa mwanafunzi na kwa jinsi ambayo amekua akifanya kwa muda mrefu na brand na yeye kama mwanamuziki kuzidi kukua nadhani na wao pia waliona fursa ya kufanya nae ushirikiano ili waweze kumuwezesha zaidi ili waweze kushinda WOTE.

Yangu matumaini kama ada uta enjoy episode hii na kujifunza zaidi.
Love,
Salama.

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible &...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

posted by cadillacah0